WILAYA ya Songea imeadhimisha Sherehe ya Uhuru wa Miaka 61 Tanzania Bara kwa mdaharo wa mada 6.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema amewakilishwa na Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano ametoa rai kwa Watanzania kuhakikisha wanalinda uhuru wa Nchi.
“Uhuru unalindwa kwa kufanya kazi na matatizo yoyote yatakayo jitokeza yanatatuliwa na Watanzania wenyewe”.
Afisa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Songea Lucy Mbalue akiwasilisha mada ya Elimu na Afya amesema kabla ya Uhuru Wilaya ya Songea ilikuwa na Shule za Sekondari 2 na Shule za Msingi 17.
Amesema kwa kipindi cha miaka 61 ya Uhuru sekta ya Elimu ilipiga hatua kubwa kwa Wilaya ya Songea inashule za Msingi zinazomilikiwa na Serikali 205 na Sekondari 76.
Hata hivyo kwa upande wa Afya kabla ya Uhuru Wilaya ya Songea ilikuwa na Hospitali 2 na baada ya Uhuru Wilaya ina Hospital 3 vituo vya Afya 17 na Zahanati 75 na zingine kama Hospital Vituo vya Afya na Zahanati zinaendelea kujengwa na kukamilishwa.
Kwa upande wake Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Joseph Mrimi amesema kipindi cha miaka 61 ya Uhuru katika Sekta ya Kilimo imeendelea kufanya vizuri kwa kuongeza pato la Taifa na kuongeza uchumi na kuleta maendeleo.
“Sisi Mkoa wa Ruvuma kuanzia msimu uliopita miaka mitatu kurudi nyuma tumeongoza kitaifa kwa uzalishaji wa Chakula ikiwemo Wilaya ya Songea imechangia kwa kiasi kikubwa”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Desemba 9,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa