MIAKA 61 ya Uhuru Tanzania Bara imeleta mafanikia makubwa katika Sekta mbalimbali na kusababisha maendeleo Makubwa.
Hayo yametajwa katika Sherehe za Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Miaka 61 Tanzania Bara iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Daniel akitoa utangulizi katika Sherehe hizo amesema Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa Wajerumani walitawala Tanganyika kama sehemu ya kujipatia malighafi bila kuweka miundo mbinu ya kutosha.
Hata hivyo amesema miundombinu iliyowekwa ilikuwa nikwaajili ya manufaa yao na watumishi wake na ilikuwa michache sana.
Juma Nyumayo akiwasilisha mada ya Siasa na uongozi katika Sherehe hizo amesema Uongozi ni majukumu ya kufanyamaamuzi na kushughulika na maswala yako au watu wengine bila kuwa chini ya mamlaka nyingine.
Nyumayo amesema kabla ya mwaka 61 wajerumani waliwaona watanganyika kama wanyama,waliwadhalilishwa na kuona kama hawana hakili wala haki ya kuishi pamoja na kumiliki.
“Mungu akajalia Kupitia uongozi wa Rias wa Awamu ya kwanza Julias Kambalage Nyerere na vyama vya kisiasa alihamasisha nchi nzima tukapata Uhuru wetu mwaka 1961”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Desemba 9,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa