MKUU wa Shule ya Sekondari ya Madaba Kelvin Kalesa amezitaja changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Hayo amesema katika maafari ya 12 ya kidato cha sita ikiwa changamoto hiyo ni pamoja na upungufu wa viti na meza,projector, computer na ukarabati wa kiwanja cha michezo.
Hata hivyo kalesa ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia kwa jitiahada zinazofanyika kwa kukarabati miundombinu mashuleni ikiwemo shule ya Sekondari Madaba day.
“Tukushukuru wewe Mbunge wetu wa Jimbo la Madaba kwa kazi kubwa unayoifanya sisi ni kati ya wale waliofanikiwa kwa kupata madarasa mapya na mengine kukarabatiwa katika shule ya Madaba day”.
Naye Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama akiwakilishwa na Meneja wa Shamba la Miti Wino Grory Fotunatus ameahidi kutatua changamoto hizo kwa wakati ikiwa katika shule nyingi amenunua vifaa hivyo.
Kwa upande wake Meneja wa shamba la Miti wino amesema watashirikiana na Mbunge kutatua changamoto zilizojitokeza katika Shule hiyo na atahakikisha wananunua jezi za michezo na mipira.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Aprili 19,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa