TANZANIA ni nchi ambayo inahifadhi nyingi za wanyamapori, Mkoa wa Ruvuma ni Miongoni mwa hifadhi za Wanyama pori wenye sifa ya kujamiiana kwaajili ya uzazi tu.
Akizungumzia Mnyama aina ya Twiga afisa maliasili Msaidizi kituo cha Taarifa za Utalii Mkoa wa Ruvuma ABdallah Omary Ambani amesema ni mnyama anayejamiiana kwa sekunde 3 na kupumzika kwa masaa 2 na kurudia tena sekunde 3 na kubeba mimba miezi kumi na nne mpaka kumi na tano na kuzaa mtoto 1
Amesema mnyama huyo anajamiana kwa mda mfupi kwa sababu anashinikizo la damu na akijamiiana kwa mda mrefu anaweza kuhatarisha maisha yake na analala kwa dakika ishirini, kutokana na tabia hiyo kumpelekea kuishi kwa mda wa miaka 25 mpaka 40.
“Twiga anazaa mtoto ambae anajiweza baada ya kuzaliwa anakaa dakika kumi na tano mpaka ishirini kuanza kutembea kutokana na mazingira anayoishi anamaadui wengi sana,inaweza kupekea kupungua kwa wanyama hao”.
Amesema wanyama hao katika Mkoa wa Ruvuma wanapatikana katika hifadhi ya Liparamba,Gesi Masoa,Hifadhi ya Nyerere na Litumbandyosi
Ambani amesema mnyama huyo licha ya sifa hiyo anasifa nyingi nyingi katika maisha yake ikiwemo kuwa na viungo virefu na kuwa na pembe zenye nywele na zinamsaidia kuchukua hewa angani na kupeleka kwenye mishipa yake ya damu pia kupambana na maadui.
Amesema Twiga anaupekee wa kuishi katika miti ya Migunga na miti hiyo inamiba mingi kupitia mdomo wake uliochongoka na pua yake imeziba inamsaidia kula majani ya mti huo bila kupata madhara yoyote.
Hata hivyo ameendelea kumwelezea mnyama huyo kuwa ana Ulimi mrefu na Mgumu unamwezesha kutopata madhara anapokula majani kwenye miti hata kwenye macho yake yana nundu zinamsaidia kutochomwa na miiba hiyo anapokuwa anakula.
Afisa maliasili msaidizi amesema mnyama huyo kutokana na urefu wake hupendelea kula miti mirefu na majani ya katikati na inampelekea kutokunywa maji mara nyingi kutokana na chakula anachokula ikiwa wanyama wengine kunywa maji zaidi ya mara 5 kwa siku.
“Mnyama huyo miguu yake ni mirefu inamsaidia kupambana na maadaui anapiga mateke mbele na nyuma anaweza kumuua hata Simba pia ni mnyama mpole lakini akichokozwa anakuwa mkali,na mkia wake ni mrefu humsaidia kufukuza wadudu wanaotua katika mwili wake”.
Akielezea kuwa mnyama huyo anapoenda kunywa maji wanakuwa kundi lakini wanakunywa kwa kusubiliana ili kujilinda dhidi ya maadui na wanapenda kujichanganya na wanyama waaina nyingine wanapokuwa katika matembezi ili kujua kama kuna maadui.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Desemba 28,2020.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa