SHULE ya Msingi Mkwera Kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba inajumla ya wanafunzi 605 na inawalimu 8.
Akisoma taarifa katika Mahafari ya darasa la saba leo Septemba 22,2023 Faraja Mkorongo kwa mgeni ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama aliyewakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Teofanes Mlelwa.
Mwanafunzi huyo amezisema changamoto mbalimbali zinazowakabili katika Shule hiyo ikiwa ni pamoja na uhaba wa viti na Meza kwa walimu kupelekea kukalia madawati ya wanafunzi,Printer na Fotokopi Mashine pamoja na mapaa ya Majengo hayo kuchakaa.
Mgeni rasmi akijibu Lisala hiyo amechangisha harambee kupitia kunadisha keki na kupatikana shilingi Laki nne na theletuni kwaajili ya kuboresha mapaa ya shule,pia ameahidi kuleta rangi na mashine ya kutolea kopi pamoja na Printa ifikapo Octoba mwaka huu 2023.
Hata hivyo Meneja wa Shamba la miti Wino Grory Kasmiri akiwakilishwa na Geofrey Shio ameahidi kutatua changamoto ya Viti na Meza za Walimu katika Shule ya Msingi Mkwera.
Moja kati ya wazazi wa Wanafunzi hao Jonisia Kihega akizungumza katika hafra hiyo amewashukuru walimu na kuwapongeza kwa kuwapa uhuru wa kuja Shuleni hapo mara kwa mara kuangalia maendeleo ya Wanafunzi na kupelekea Shule hiyo kufanya vizuri katika Mitihani ya Kitaifa.
“Walimu wa hapa Mkwera wanaumoja sana ukija hapa wanakupokea kwa tabasamu ndiomana hata sisi wazazi tuna wapa ushirikiano unaotupa uhuru wa kuwaangalia watoto hao kwa pamoja”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa