MBUNGE wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama akiambatana na viongozi wa chama cha Mapinduzi amekabidhi vifaa tiba vikiwemo vitanda 10 vya kujifungulia vilivyotolewa kupitia mchango wa wambunge katika hospitali ya Wilaya ya Madaba.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mussa Rashid amesema hospitali hiyo imejengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni tatu.
“Hii ni moja ya taasisi kubwa sana katika halmashauri yetu,Rais Samia Suluhu Hassan ametuwezesha na imetokana na Mbunge wetu mchapakazi na Madiwani wetu”
Imeandaliwa na Aneth ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 18,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa