Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amewataka viongozi na Wataalamu Mkoani Ruvuma kuhakiksha wanafanya ukaguzi wa nyaraka za miradi yote itakayotembelewa na mwenge ili kujiridhisha na hatua ya utekelezaji wa mradi husika.
Amesema kila kiongozi katika nafasi yake anapaswa kuwajibika katika kutekeleza majukumu yake ya kazi ikiwemo na kujenga ushirikiano katika kusimamia miradi yote inayotekelezwa ngazi ya Halmshauri na kufikia lengo lililokusudiwa.
Hayo yamejili katika kikao cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Mkoani Ruvuma kilichofanyika leo tarehe 24 Februari katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambapo kilihudhuriwa na viongozi ngazi ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Mkatibu tawala Wilaya, Wakurugenzi wote, Waratibu wa Mwenge kila Halmashauri, pamoja na kamati ya ulinzi na usalama, kilichofanyika kwa lengo la kupokea tathimini ya Mbio za mwenge wa Uhuru 2022 na maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2023.
Kanal. Laban amesema Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 Mkoani Ruvuma zitaanza rasmi tarehe 17 Aprili 2023, ambao Mwenge utapokelewa ukitokea Mkoa wa Lindi na mapokezi yatafanyika katika kijiji cha Sauti Moja, Wilayani Tunduru ambapo utakimbizwa katika Halmashauri 8 nane na kukabidhiwa katika Mkoa wa Njombe kijiji cha Kipingu tarehe 25 Aprili 2023.”Alibanisha”
Kwa mwaka 2022 Mkoa wa Ruvuma ulipokea Mwenge wa Uhuru tarehe 08 April 2022 katika kijiji cha Lituhi Wilaya ya Nyasa na ulikabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Mtwara tarehe 16 April 2022 katika kijiji cha Lumesule Wilaya ya Nanyumbu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amesema Chama cha Mapinduzi kina wajibu wa kutembelea miradi na kufanya ukaguzi wa miradi yote inayotekelezwa na Serikali ili kujiridhisha kila hatua ya mradi katika Halmashauri.
Komredi Oddo amewataka wataalamu wte Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanaweka kumbukumbu za kila mradi ambao utatembelewa na Mwenge ili kujirisha na utekelezaji wake.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa