Mratibu wa Mradi wa BOOST Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Raphael Kibirigi ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia kwa kuwezesha walimu wa awali kupata mafunzo yakuwajengea uwezo katika ufundishaji na ujifunzaji.
Kibirigi amesema mafunzo hayo yatawasaidia walimu hao kwa namna bora ya kufaragua na kutengeneza zana na kumudu miongozo na kuisimamia amabyo inasimamia elimu ya awali.
“Mara baada ya mafunzo haya walimu watakuwa chachu ya kufikisha ujumbe kwa walimu wengine na watafuata taratibu zote za ufundishaji wa elimu ya awali kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili itafanyika katika shule zote”
‘‘Tuishukuru sana Serikali ya awamu ya Sita ambayo imeona jambo hili na kutuletea sisi watu wa madaba, ili tuweze kufikia malengo yaliyokusudiwa”
Kwa upande wake Mkufunzi ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Lilondo Goreth Chales amesema kupitia mafunzo waliyopata kwa mda wa siku tatu wanatarajia kutoa elimu thabiti kwa walimu wa awali.
Amesema kupitia mafunzo anatarajia kuona mabadiliko yakianza katika utekelezaji wa elimu ya awali kwa wadau ngazi shule pamoja na wadau wengine ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa la mafunzo hayo kupitia mradi wa BOOST.
Kutoka Kitengo cha Mawasilino Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 18,2025.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa