Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametoa rai kwa Makarani 22 waogozaji wapiga kura kutokuwa na upendeleo wa chama katika kituo cha kupigia kura.
Hayo ameongea alipofungua mafunzo ya siku moja ya Makarani waongozaji watakao simamia uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Mtyangimbole na kuwa apisha kiapo cha kutunza Siri katika zoezi la uchaguzi.
Mkurugenzi amesema mafunzo hayo yanalenga kutoa maelekezo ya namna ambavyo karani mwongozaji anavyotakiwa kutekeleza majukumu yake katika kituo cha uchaguzi .
Hata hivyo amesema Makarani hao wamepewa kazi hiyo kwa kuzingatia weledi na uaminifu walionao kwa wananchi watakao jitokeza kupiga kura.
“Sitegemei miongoni mwenu kwenda kinyume na maelekezo yatakayotolewa na wasimamizi wa uchaguzi mzingatie kwamba mmekula kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama”.
Mohamed ametoa rai kwa Makarani hao kuwa makini na wasikivu na waelevu katika kuhakikisha wanaelewa maelekezo wanayopewa na wasimamizi wa uchaguzi.
Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zakia Mohamed Abubakari alipoongea na Makarani hao amesema katika zoezi hilo la uchaguzi wawe waadilifu watakapo kuwa eneo la Uchaguzi pamoja na kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 15,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa