• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MAKAMU wa Rais kuzindua kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya mama Samia Ruvuma

Posted on: July 19th, 2023

Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt.Philipo Mpango anatarajia kuzindua kampeni ya kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Julai 22 mwaka huu katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakati anazungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea.

Amesema mara baada ya uzinduzi wa kitaifa,kampeni hiyo inatarajia kufanyika kwa siku kumi kisha kuendelea hadi Desemba 2023.

Hata hivyo amesema kampeni hiyo inatarajia kufanyika katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma ambayo itahusisha kata 80 na vijiji 238.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Songea mjini Dkt.Damas Ndumbaro ameitaja Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kuwa inalenga kulinda na kukuza haki ya upatikanaji haki kupitia huduma za msaada wa kisheria nchini.

“Kampeni inatarajia kuboresha upatikanaji wa haki kwa watu wasiojiweza hususan wanawake,Watoto na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu,kampeni itachangia kuimarisha amani na utulivu na kuleta utengamano wa kitaifa’’,alisisitiza.

Dkt.Ndumbaro amesema kampeni hiyo inatarajia kufanyika kwa miaka mitatu kuanzia Machi 2023 hadi Februari 2026 na kwamba kampeni inafanyika katika nchi nzima kwenye mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar kwa kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi.

Amebainisha zaidi kuwa elimu ya kisheria italenga katika masuala ya ukatili wa kijinsia,migogoro ya ardhi,mirathi,usuluhishi kwa njia  mbadala,mifumo ya kisheria na masuala yahusuyo haki za binadamu kwa ujumla.

Kumekuwa na ongezeko la wananchi waliopata huduma ya msaada wa kisheria hapa nchini ambapo takwimu za hivi karibuni zinaonesha  katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2022,jumla ya watu 41,924 walipatiwa huduma ya msaada wa kisheria kati yao wanaume 17,068 na wanawake 24,856.

 

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa