MAHANJE SACCOS wamefanya Mkutano mkuu na kupitisha bajeti ya mwaka wa Fedha 2023/2024 ya shilingi Milioni 156 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akizungumza katika mkutano huo Meneja wa Mahanje SACCOS Kassim Masengo amesema mwaka 2022 walikuwa na bajeti ya mapato na matumizi shilingi Milioni 120 walifanikiwa kutumia shilingi Milioni 105.
“Leo tulikuwa na mkutano mkuu wa wanachama hiyo ni kutimiza sheria ya ushirika juu ya kufanya mkutano wa mwaka”.
Hata hivyo Masengo amesema katika mkutano huo wamefanya uchaguzi wa mjumbe mwakilishi wa mkutano mkuu uchaguzi wa wajumbe wa bodi,kamati ya usimamizi Kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kwa upande wake Afisa ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sadam fupi akiwakilisha Ofisi ya Mkurugenzi Madaba,Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Ruvuma wa tume ya maendeleo ya ushirika pamoja na mrajisi mkuu Dodoma katika kusimamia zoezi nzima la uchaguzi huo.
Afisa Ushirika ametoa rai kwa viongozi waliochaguliwa kuhakikisha wanakuwa waaminifu ikiwa wanancha wamewachagua kwa kuwaamini.
“wananchama wamewaamini hakikisheni mnaendelea kuwa waaminifu muwe wafuatiliaji, nina amini tutashirikiana kama tulivyoshirikiana kwa mda wa miaka mitatu iliyopita”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa