SHULE ya Sekondari Lipupuma Halmashauri ya Madaba wametatuliwa changamoto ya Matenki Mawili ya kuhifadhia maji yenye thamani ya shilingi Milioni 2.
Akisoma taarifa Mkuu wa Shule hiyo Gofrid Nyingo katika Mahafari ya Kidato cha nne Mwaka 2023 na kuzitaja changamoto zinazokabiliwa na Shule hiyo.
Nyingo amesema changamoto hizo ikiwa ni pamoja na uhaba wa maji wanafunzi wanahangaika kujitafutia maji kutokana na maji machache yanayopatikana eneo la Shule,ukosefu wa bweni la wavulana ambapo kwa sasa wanalala katika moja ya darasa,ukosefu wa bwalo la chakula kipindi cha mvua wanafunzi kukosa eneo la kulia wanafunzi.
“Kwa kipindi cha mwaka wa Fedha 2022/2023 tumekuwa na mafanikio kwa kupewa fedha ya mapato ya ndani zaidi ya shilingi Milioni 8 kwaajili ya ujenzi wa matundu 8 ya vyoo vya wanafunzi wa kiume ambao hawakuwa na vyoo kabisa”.
Mgeni rasmi katika Mahafari hayo Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amewakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Teofanes Mlelwa ametatua changamoto ya ununuzi wa tenki 1 kwa kusaidiana na Wazazi kwa kunadisha keki.
Hata hivyo Mwenyekiti amesema Tenki moja litanunuliwa na wadau wa Shamba la Miti Wino TFS Halmashauri ya Madaba.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 6,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa