WANAFUNZI 92 wa Stashahada ya Afya ya Wanyama na uzalishaji wamehitimu katika chuo cha Lita Halmashauri ya Madaba.
Moja ya wahitimu Geofrey Kayangea kisoma Risala kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama akiwakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa amesema walianza mwaka wa masomo 2019/2020 jumla ya wanafunzi 102 hadi mwaka huu wa masomo 2022/2023 wamehitimu wanafunzi 92.
Kayange amesema mafanikio yaliyojitokeza ikiwemo kuhitimu kwa idadi kubwa sawa na asilimia 91.2 kuungana na kusaidiana na wengine walipokuwa na changamoto ya misiba, kukosa ada,kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji pamoja na kuwa na ligi za michezo na kuwa washindi wakwanza katika michezo mbalimbali.
Hata hivyo amezitaja changamoto zilizojitokeza baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo na kushindwa kutimiza ndoto zao,upungufu wa vifaa vya michezo,ujenzi wa daraja la mto mkwese ilikurahisisha kufika Madaba na chuoni,Kisima kirefu cha Maji kwa matumizi ya wanafunzi na watumishi pamoja na mifugo.
Katika Hafla hiyo Mlelwa amejibu changamoto hizo ikiwa Serikali kufanyia kazi suala la ada kwa wanafunzi iliwaweze kupata mikopo ikiwa wanafunzi wanashindwa kumaliza masomo yao kwasababu ya kushindwa kulipa ada.
Hata hivyo Mwakilishi wa Mbunge amesema kuwa ifikapo Octoba mwaka huu 2023 atapeleka vifaa vya michezo katika chuo hicho.
“Daraja la mto mkwese ninauwezo nalo nitakuja na Mhandisi ili mnielekeze ,kama limeshindwa kufanyiwa kazi kwa kipindi hiki mwakani litatengenezwa,pamoja na kisima kirefu nitakuja na meneja wa RUWASA tuwasikilize”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 27,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa