WARATIBU wa Lishe Halmashauri yaWilaya ya Madaba wamepewa mafunzo ya utoaji wa huduma za Lishe ikiwemo huduma ya mtoto,wajawazito na wazee kwa vituo vyote.
Akizungumza mara baada ya Mafunzo hayo Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo Neema Bernad amesema mafunzo hayo yatawawezesha waratibu kukusanya taarifa ya utoaji wa huduma za Lishe zinazotakiwa kutolewa pamoja na kutoa Elimu kwa jamii.
Hata hivyo amesema mafunzo hayo nikwaajili ya kuboresha hali ya Lishe katika maeneo ya Halmashauri Pamoja na kutathimini hali ya Lishe na kukusanya takwimu sahihi kwa Watoto wadogo,wajawazito Pamoja na wazee.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Agosti 16,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa