MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amefunga mafunzo ya Makarani yaliyofanyika kwa siku moja na amewaomba kuzingatia yote yaliyofundishwa.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba amewapongeza wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo pamoja na Maafisa kutoka Tume ya Uchaguzi kwa ushirikiano ulioonyeshwa kwaajili ya kutoa mafunzo hayo kwa Makarani.
“Mkasimamie zoezi la uchaguzi kwa weledi kama mlivyofundishwa pamoja na kuwa makini katika zozi hili la Kitaifa tutangulize Maslahi ya Taifa Mbele”.
Hata hivyo amesema Makarani hao watakapo kuwa katika eneo la kituo cha uchaguzi wazingatie kuwa nadhifu pamoja na kujiamini kupitia maarifa waliyo patiwa na wasimamizi wasaidizi wa Jimbo.
“Najua asubuhi mmekula kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza Siri tunaamini mtaenda kujiamini pamoja na kuwa na Lugha ya staha kwa wapiga kura”.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zakia Mohamed Abubakari mara baada ya mafunzo hayo kumalizika amewapongeza Makarani waongoza wapiga kura kwa mafunzo usikivu na uelewa wa haraka.
Hivyo Kamishna amesisitiza kuwapa kipaumbele wenye mahitaji maalum na kutojisahau wanapokuwa katika kituo cha uchaguzi.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 15,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa