HALAMSHAURI ya Madaba imekuwa na mafanikio mbalimbali katika utekelezaji wa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Idara ya Mipango Prosper Luambano katika Kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitisha Bajeti ya 2023/2024.
Luambano amesema mafanikio hayo ya utekelezaji wa Bajeti 2021/2022 ni pamoja na uimalikiaji wa hali ya ulinzi na usalama katika vijiji 22 na kata 8 za Halmashauri,kuratibu na kuendesha vikao vyote vya kisheria ngazi ya Wilaya yakiwemo mabaraza 6 vikao vya kamati ya kudumu na vikao vya menejimenti ya Halmashauri.
Amesema mafanikio mengine wamepokea watumishi wa ajira mpya kwa idara ya utawala12,Elimu 8 na Afya 11 pamoja na watumishi 66 wamepandishwa vyeo na 37 wamebadilishwa muundo.
Luambano amesema kwa upande wa idara ya Afya kwa kipindi cha Julai 2021 hadi 2022 Halmashauri imefanikiwa kupokea zaidi ya shilingi billioi 2 kwaajili ya utekeleza wa shughuli mbalimbali katika sekta ya Afya.
Amesema Hospitali ya Wilaya ya Madaba milioni 800 imepokekelewa kwaajili ya ujenzi wa Hospitali pamoja na ujenzi wa kichomeo taka jengo la kufulia na ukamilishaji wa majengo ya awali,mionzi,jengo la stoo ya Dawa,jengo la maabara na jengo la wagonjwa wa nje OPD.
Hata hivyo amesema kiasi cha shilingi milioni 300 imetolewa kwaajili ya huduma ya dharula na shilingi milioni 90 kwaajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya pamoja na vituo vya afya milioni 500 zimetolewa kutokana na fedha ya tozo kwaajili ya kituo cha Afya Matetereka.
Pia amesema kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 122 imetolewa kwaajili ya utekelezaji wa mradi endelevu wa maji na usafi wa mazingira vijijini kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya 4 Mbangamawe,Mateteleka,Igawisenga na Kituo cha Afya Mtyangimbole.
Milioni 150 imepokelewa kwaajili ya ujenzi wa Zahanati 3 Mbangamawe,Magingo na Kipingo pamoja na ununuzi wa Dawa na Vitendanishi imepokelewa zaidi ya shilingi 181 na Halmashauri katika mwaka wa fedha 2021/2022 imefanikiwa kutoa huduma ya chanjo mkoba katika vituo 16 vya kutolea huduma ya Afya vijijini.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Februari 7,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa