AFISA Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Mariam Juma ametoa Elimu ya mpango wa Taifa ya Malezi na makuzi ya awali ya Mtoto katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akizungumza katika Baraza hilo amesema mpango huo unasimamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii jinsia wanawake na makundi maalum na ilizinduliwa na Waziri Doroth Ngwajima Mwezi Disemba 2021 Dodoma kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema Mpango huo unafanyika katika Mikoa yote 26 ukiwemo Mkoa wa Ruvuma ulianza kutekelezwa mwaka 2022 ikiwa ni mpango wa miaka 5 kuanzia 2021 /2026.
Juma ameeleza lengo la mpango huo ni kutoa huduma ya afya,Lishe, malezi yenye mwitikio,ujifunzaji wa awali kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0-8,kuimarisha ushirikiano kwa wadau katika sekta mbalimbali na kutoa huduma za mama.
“Ukuaji wa mtoto unaanza tangu anapokuwa tumboni hivyo wazazi na Serikali tunajukumu la kuhakikisha chanjo zote zinapatikana,malezi yenye mwitikio kuzungumza na mtoto anapokuwa tumboni,amani nyumba,Lishe bora,ujifunzaji wa awali”.
Hata hivyo amesema asilimia 90 ya mawanadamu inatengenezwa kuanzia miaka 0-8 na asilimia 10 inatengenezwa kuanzia miaka 8 na kuendelea .
“Hivyo ni kipindi muhimu cha kuwekeza kwa wazazi na wadau wengine kwa ujumla wake”.
Amesema kwa kipindi cha miaka 0-8 mtoto anatakiwa kupewa malezi bora hatakiwi kufanyiwa ukatiki kwa kupigwa,kusikia,na kuhisi.
Amesema katika kuzingatia vitu vya msingi katika malezi na makuzi ya mtoto kuna Lishe Bora,Kucheza,kupumzika,kupata maji safi na salama ya kunywa,Afya Bora ,ulinzi na Usalama,uchangamshi wa awali na vifaa vya michezo.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 31,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa