IDARA ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto Halmashauri ya Madaba kwa mwaka wa fedha 2021/2022 imetoa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani jumla ya zaidi ya shilingi milioni 67 kwa Vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Afisa mipango Halmashauri ya Madaba Prosper Luambano ametoa taarifa hiyo katika kikao cha bajeti cha Baraza la Madiwani kuwa Halmashauri kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 ilipanga kutumia Zaidi ya shilingi milioni 319 ya makusanyo ya fedha za mapato ya ndani.
Luambano amesema kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi milioni 79 ilpangwa kwaajiliya kutoa mkopo kwa makundi ya wanawake,vijana na wenye ulemavu.
“Hadi kufikia 30 Juni,2022 Halmashauri ilikusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 677 sawa na asilimia 86 ya lengo”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 9,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa