HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya HPV dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wa shule za msingi na Sekondari kuanzia miaka 9-14.
Zoezi hilo limezinduliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed aliyewakilishwa na Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Philemoni Namwinga katika Shule ya Msingi Kifaguro.
Namwinga akizungumza katika zoezi hilo amesema lengo la chanjo zote ni kujenga jamii yenye Afya, ikiwa kauri mbiu ni jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya.
Kwa upande wake Mwakikili kutoka OR-Tamisemi Dr. Manyanza Mponeja amesema mpango wa chanjo hiyo ni kuwakinga watoto ambao hawajaanza kufanya ngono wenye umri wa miaka 9-14 na ugonjwa huo unatokana na kutofanya tohara kinga kwa wanaume.
“Naomba nitoe wito kwa wazi kuhakikisha watoto wa kiume wanafanyiwa tohara salama inasaidia kukinga maambukizi kwao hasa HIV na kuwa msafi”
Mponeje amesema zoezi hilo litafanyika kuanzia Aprili 22 hadi Aprili 26 kwa kuhakikisha wanafikia asilimia 80 ya watoto waliochanjwa.
“Chanjo hii siyo mpya ikiwa mabadiliko inatolewa mara moja na kushusha umri ilikuwa inatolewa miaka 14 na kuendelea kwa sasa inatolewa kuanzia miaka 9 na haina changamoto yoyote ilianza kuanzia mwaka 2014 ”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Aprili 22,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa