Timu ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamezungumza na kikundi cha ufyatuaji wa tofari cha kwetu Madaba kuhusu uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake
Akizungumza Anita Makota amesema Jukwaa la Wanawake liliundwa kwaajili ya kushirikisha wataalamu mbalimbali .
Amesema lengo la uundwaji wa jukwa hilo, Wanawake walikuwa hawana sauti ya kuongea hivyo kupitia jukwaa hilo lilipelekea kupeana fursa mbalimbali za kibiashara na kutatua changamoto kwa pamoja.
“ Halmashauri ya Madaba Jukwaa liliundwa mwaka 2021 lakini lilikuwa halijaanza kufanya kazi tarehe 28 tunatarajia kuwa na ugeni mkubwa sana kwaajili ya Uzinduzi“.
Hata hivyo amesema Jukwaa hilo litazinduliwa rasmi tarehe 28 Septemba 2023 pamoja na maonyesho ya biashara Mbalimbali za wajasiriamali.
“Hakutakuwa na vikundi tu hata UWT wanashughuli zao zitaonyeshwa siku hiyo tujitokeze kwa wingi kila mmoja na biashara yake”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 31,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa