HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya kikao cha utekelezaji wa afua za Lishe robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 na robo ya kwanza ya Mwaka wa fedha 2023/2024.
Afisa Lishe wa Halmshauri hiyo Jovenart Ntelagi amesema zoezi la kupambana na lishe duni kwa watoto chini ya miaka mitano wamehakikisha Lishe bora inazingatiwa kwa makundi yote muhimu na kuepuka matatizo yanayotokana na lishe duni.
“Tumeendelea kutoa unasihi wa lishe bora kwa akina mama wajawazito wanaonyonyesha na wazazi/walezi wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano”.
Ntelagi amesema jumla ya watoto 3060 wenye umri wa chini ya miaka mitano wamepimwa hali ya lishe kati ya watoto hao 69 sawa na asilimia 2.25 waligunduliwa kuwa na changamoto katika hali zao za lishe.
“Watoto 4 kati ya watoto 69 waligunduliwa kuwa na utapiamlo mkali,watoto 65 waligunduliwa kuwa na utapiamlo wa kadri”.
Amesema watoto waliogundulika kuwa na utapiamlo wa kadri walipewa unasihi wa uandaaji wa chakula na ulaji unaofaa na wale waliokutwa na utapiamlo mkali walipewa rufaa ya kwenda kutibiwa hospitali ya Mkoa .
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Disemba 8,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa