Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Madaba kwa kusimamia vizuri swala la Lishe.
Hayo amesema katika Kikao cha Lishe cha robo ya tatu mwaka 2023/2024 huku wakiwa na maadhimio matano ya utekelezaji.
“Halmashauri ya Madaba hatuna tatizo ambalo litatufanya tukashuka katika swala la lishe, kiufupi tunafanya vizuri kwa sababu sisi wenyewe tunaushirikiano mzuri tunajitambua”.
Hata hivyo mwampamba amesema katika kikao hicho wameadhimia watoto wenye utapia mlo mkali watibiwe katika Hospitali ya wilaya na mazingira yaandaliwe ili matibabu yaweze kufanyika.
Amesema shule zote za Msingi na Sekondari wahakikishe wanapanda mbogamboga badala ya kupanda maua itasaidia watoto wanapata virutubisho vya Lishe pale watakapokuwa wanakula hivyo wajifunze kwa vitendo.
“Watendaji wa Kata waendelee kutekeleza sheria ndogo za kuhakikisha wazazi wanachanga chakula katika shule zao”.
Mwampamba amesema kila shule wahakikishe wanabadili mfumo badala yake watumie mahindi na maharage lishe na kuendelea kutafuta virutubisho vya kuchanganya katika chakula pamoja na kuchawishi wazazi walime mahindi na maharage Lishe.
“Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji tusiwe tunaweka mtindo mmoja wa kumwonyesha mwanakijiji kunywa uji tu tuchanganye chakula tuwe wabunifu kwa vyakula tofauti”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 9,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa