HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya Mkutano maalum wa baraza la madaiwani wa kufunga hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2024.
Katika baraza hilo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amesema katika mapendekezo yote yaliyotolewa kuwa katika mwaka mpya wa fedha 2024/2025 wamejipanga kukusanya mapato ya ndani.
“Hatutaweza kulipa madeni kama hatuna makusanyo mazuri mimi na menejmenti yangu tumejipanga ipasavyo kuhakikisha kwamba baadhi ya maaeneo tunayafanyia kazi hasa katika kupata vyanzo vya mapato vya kudumu”.
Hata hivyo Mohamed amesema katika halmashauri hiyo wanatarajia kupata fedha kwaajili ya ujenzi wa stendi kupitia mradi wa TASAF ambapo itapelekea ukusanyaji wa mapato kwa Wingi.
“Tumesha andika andiko makao makuu na tunatarajia kujenga kwa kushirikiana na wananchi waliojenga vibanda na kuepukana na adha ya kutoka katika utegemezi”.
Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mwaka wa fedha 2023/2024 ilikusanya zaidi ya bilioni moja sawa na asilimia 90 ya makisio ya bajeti.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa