HALMASHAURI ya Madaba imedhamilia kuondoa sifuri Sekondari baada ya kuweka historia ya kufanya vizuri miaka mitatu mfurulizo.
Akizungumza katika balaza la Madiwani katika kikao cha robo mwaka Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha Pili mika mitatu mfurulizo.
Hayo amezungumza katika Balaza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi na kuwakumbusha kamati ya Elimu kufanya tathimini kila mara na kutatua changamoto ili kutokomeza alama ya sifuri kwa kidato cha pili na cha nne.
Mgema akirejea kikao cha tathimini ya Elimu kilichopita maagizo aliyoacha madaba kwa wataalam wa kamati ya Fedha na Elimu inawapasa kufanya tathmini ya utekelezaji na mkakati wa kuendelea kushinda.
“Tufanye tathmini ya kiutekelezaji kwaajili ya kujiwekea mikakati matokeo ya kidato cha pili mwaka jana 2020 bado kunawatoto 18 ambao wamepata sifuri na kuna watoto 26 wamepata sifuri hao ndi wametufanya tushuke chini lakindi kidato cha sita wamefanya vizuri“.
Amesema mkakati wa kuondoa sifuri kwa kidato cha pili na cha nne zipangiwe mkakati na ajenda zipelekwe kwenye kamati ya Elimu na Kamati ya Fedha na ziingizwe kwenye Balaza ili mikakati ya kuondoa sifuri ifanye kazi,bila kusingizia upungufu wa walimu.
Amesema moja wapo ya mikakati inayotakiwa kuwekwa ilikuondoa sifuri kufanya tathmini ya mahitaji ya miundombinu ya shule,madarasa,ofisi za walimu na samani za madarasa na ofisi za walimu kwa kuanzia.
Amesema mwaka huu kwa wale ambao hawajajiunga mwezi wa tatu tumefunga usajili taarifa tumezipeleka tamisemi ili waweze kutupatia fedha kulinga na idadi ya wanafunzi waliopo kwenye mfuko wa Elimu bila malipo na tukifunga usajili tunajua idadi ya wanafunzi walioopo ,vyumba vya madarasa vinalingana na wanafunzi waliopo, Na madawati viti na meza vinalingana na idadi ya watoto hapo inatupasa kuweka mikakati ngazi ya Halmashauri .
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Mei 3,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa