• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MAAFISA Ugani 34 Ruvuma wapatiwa mafunzo ya upimaji wa afya ya udongo

Posted on: May 20th, 2022

AFISA Elimu Mkoa wa Ruvuma Emmanuel Kisongo  amemwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki kufungua mafunzo ya  maafisa ugani 34  ya maandalizi ya upimaji wa afya ya udongo .

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Kisongo amesema wataalam wa kilimo ngazi ya Kata na vijiji mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kutekeleza zoezi la upimaji wa udongo litakalofanyika katika vijiji 100 ndani ya Mkoa wa Ruvuma.

Kisongo ametoa rai kwa maafisa kilimo waliopata mafunzo hayo wakasimamie na kutekeleza kwa weledi zoezi la upimaji wa afya ya udongo kwa ujumla wake hususani katika vijiji vitatu hadi vine kwa kila afisa kilimo.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa pikipiki 7000 kwa maafisa ugani wa Kata na Vijiji kwa nchi nzima,Mkoa wa Ruvuma  tumepata pikipiki 282”.

Amesema maafisa ugani wa Kata na Vijiji wa Mkoa wa Ruvuma kila mmoja atapata pikipiki moja na seti ya  vifaa vya kutolea huduma  za ugani katika zoezi la kutambua afya ya udongo katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa.

Mtafiti Mkuu wa Udongo Kutoka TARI –UYOLE  Fredrick Mlowe katika mafunzo hayo  amesema zoezi hili lipokatika awamu ya tatu ya utekelezaji ikiwemo awamu ya kwanza ilikuwa Mkoa wa Mbeya na Songwe awamu ya pili Rukwa,Mbeya ,Iringa na Morogoro.

Mlowe amesema dhima ya mafunzo haya ni kwaajili ya kujenga uelewa  wa afya ya udongo katika kanda  na  matokokeo yake kushauli makampuni ya uzalishaji wa Mbolea na kutoa mapendekezo ya mazao mbalimbali na kurudi katika tija inayostahili.

Mtafiti wa afya ya udongo amesema matokeo hayo yatakuwa na kazi kumi kuwasaidia wazalishaji wa mbolea watengeneze mbolea inayoendana na hali ya maeneo  kulingana na matokeo yaliyopatikana katika upimaji wa afya ya udongo.

Kwa upande wake afisa biashara Mkoa wa Ruvuma Martin Joseph akimwakilisha Katubu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Jeremia Sendoro katika mafunzo hayo amesema baada ya upimaji wa afya ya udongo Mkoa utakuwa na kilimo chenye tija ikiwa Mkoa wa Ruvuma ni Mkoa wa Kilimo.

Amesema kwa maafisa ugani zoezi la mafunzo hayo ni muhimu ili wakashiriki kusaidia wakulima wa Mkoa wa Ruvuma waweze kujua matumizi sahihi ya mbolea ili waweze kulima kwa tija ikiwa mkoa wa Ruvuma kwa miaka mitatu mfululizo umeongozo kwa mazao ya chakula.

“ Nawaomba maafisa ugani kufanya kazi kwa uadilili  kwa maeneo sahihi ,Rais alipokuwa Tabora ameeleza mwaka wa fedha utakaanza julai kilimo ni kipaumbele cha kwanza “.

Amesema kilimo ili kilete tija wataalamu mnatakiwa mfanye vizuri  kwenye maeneo yote yanayohusika ikiwa kupima afya ya udongo,matumizi ya mbolea sahihi na kutoa elimu kwa wakulimu”.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Mei 20,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa