HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamehamasisha unywaji wa maziwa kwa wanafunzi wa darasa la awali hadi darasa la pili katika shule ya msingi Magingo.
Uhamasishaji huo umefanyika na idara ya elimu msingi,ustawi wa jamii na kilimo,uvuvi na mifugo na kugawa maziwa kwa wanafunzi 188.
Akizungumza katika zoezi hilo Afisa Mifugo kata ya Mahanje Lucy Mwaituka ametoa elimu ya unywaji wa maziwa kwa wanafunzi hao na amesema faida ya maziwa katika mwili wa binadamu.
Mwaituka amesema maziwa katika afya ya mwanadamu yanaleta avitamini D,B12 na yanaimarisha meno kwa watoto,mifupa na misuli na kusaidia kuleta kinga ya mwili.
“Ukinywa maziwa mwili wako unakuwa na kinga kamili magonjwa yanapokuja kwenye mwili wako yanakuta mwili unakinga huwezi kupata magonjwa mara kwa mara mkirudi nyumbani muwaambie wazazi wawe wanawapa maziwa “.
Naye Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo Joseph Peter amesema athali za kutokunywa maziwa kwa watoto ukiwemo ukosefu wa kalsiam na kuathiri ukuaji wa mifupa na meno na kuongeza hatari ya osteoporosi maishani.
Amesema unywaji wa maziwa hafifu hupunguza ukosefu wa protini ambayo kupelekea kuathiri misuli na na maendeleo ya tishu na upungufu wa vitamini D,B12 zinazosaidia katika mfumo wa kinga na afya ya neva.
“Ukosefu wa unywaji wa maziwa unasababisha kuharibika kwa afya ya mifupa ,ujumuishi wa chakula na kupelekea kupunguza mchakato wa mmeng’enyo wa chakula”.
Kutoka kitengo cha mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Septemba 20,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa