• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MAADHIMISHO ya Wiki ya Msaada wa Kisheria yafana Ruvuma

Posted on: November 12th, 2021

MKUU wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amefunga maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria akimwakilisha MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbaert Ibuge.

Akisoma hotuba yake katika Hafla fupi iliyofanyika katika Bustani ya Manispa ya Songea amesema Huduma ya msaada wa Kisheria inasimamiwa na Sheria ya Msaada wa Kisheria Na.1 ya mwaka 2017.

Amesema kauli mbiu ya Mwaka huu 2021 ni Maboresho Endelevu ya Haki jinai katika Kuimarisha upatikanaji wa Haki Jinai, maadhimisho hayo yamekuwa ya kipekee sana yanasisitiza matumizi na uboreshaji wa mfumo mzima wa haki jinai katika sheria zake.

Mgema ameeleza maboresho hayo  ikiwemo mbadala wa kifungo na kufanya kazi za kijamii kwa makosa ambayo si makubwa,Mkuu wa kitengo cha Polisi ana mamlaka ya kupunguza adhabu chini ya Sheria ya mwenendo wa Makosa ya jinai kifungu cha 170(6).

Amesema Dhamana ni haki ya mtuhumiwa anaposubiri shauri lake kusikilizwa anaweza kuedelea na majukumu yake ya uzalishaji wa Mali na kuinua uchumi wa Taifa.

Hata hivyo amesema faida za kutumia uangalizi wadola katika mahabusu  kusaidia kupunguza mrundikano wa wafungwa na mahabusu katika Magereza nchini ,kupunguza mashauri na kuokoa muda pale mtuhumiwa anapoamriwa kulipa faini Pamoja na kuinua uchumi wanchi  mtu akiwa huru anaweza kufanya majukumu yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kishaeria Mkoa wa Ruvuma Naomi amesema Wizara inalenga kuadhimisha Wiki ya Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na wadau wakiwemo Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa kupitia Wasajili wasaidizi wa kutoa huduma ya Msaada wa Kisheria kwa ngazi ya Mkoa.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoaka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma

Novemba 12,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa