MAADHIMISHO ya siku ya Wanawake Duniani yameziduliwa rasmi jana Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma katika viwanja vya Majimaji Mjini Songea.
Katibu wa wanawake Manispaa ya Songea Joyce Mwanja akisoma Risara kwa mgeni rasimi Gilda Siluimba Mama Askofu wa kanisa la Redeemed Mjini Songea amesema Sisi wanawake wa manispaa ya Songea tunaungana na wanawake wote Duniani hususani nchi nzima za Afrika kuzindua siku ya wanawake Duniani leo Machi 1.
Mwanja amesema Lengo la maadhimisho haya ni kutoa fursa ya kuelimisha jamii hasa wanawake kuhusu jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali,Asasi za Kiraia,Sekta binafsi na wadau wengine katika kukuza hali ya wanawake wa kitanzania.
“Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo inasema wanawake katika uongozi chachu kufikia dunia yenye usawa,kauli mbiu hii ina ukweli usiopingika kwa kuwa kabla wanawake hatujahamasika na kushika nafasi za uongozi katika miaka ya 1990”.
Hata hivyo ameipongeza Wizara ya Maendeleo ya jamii ,Afya,Wazee,Jinsia na Watoto kwa kutuletea kauli mbiu hii inayotukumbusha kuendelea kujitambua na kutambua nafasi zetu katika kuendeleza jamii kwa namna moja au nyingine.
Amesema mwaka 2020/2021 Julai hadi Desemba Songea Manispaa kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake imetolewa zaidi ya shilingi miamoja kwa vikundi 25,na zaidi ya shilingi milioni 43 imetolewa kwa vikundi 21 kwa vijana na kwa watu wenye ulemavu imetolewa zaidi ya shilingi milioni 43.
Amesema Wilaya ya Songea imeathilika na janga la UKIMWI na mikakati iliyopangwa ni pamoja na kutoa Elimu ya kupima afya kwa Hiari,kukemea mira na desturi zinazochochea maambukizi,ngoma za usiku na ulevi wa kupindukia.
Mama Askofu Gilda Siluimba wa kanisa la Rededeemed amesema katika ufunguzi wa maadhimisho hayo amewasisitiza wanawake kufanya kazi kwa bidii na kuepuka kuwa tegemezi kwa waume zao pamoja na kulea watoto katika maadili ili nchi yetu iweze kuwa na viongozi wanawake wa ngazi ya juu.
“Chachu ya kuwa na watoto wakike wanaofanya vizuri darasani inatokana na malezi ya mama,au kupata watoto wakike ambao tunatarajia wawe viongozi inatokana na mwanamke, hivyo wanawake naomba muwalee watoto katika mazingira ya kidini ili wafanye vizuri hata wakiwa shuleni na kazini na Mungu atawasaidia”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Machi 2,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa