MAKAMU Mwenyekiti wa Halmashauri Olaph Pili ambaye ni Diwani wa Kata ya Lituta ametembelea kikundi cha ufugaji wa Nyuki kinachoitwa Tuamke Yerusalem.
Katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halamashauri hiyo ameambatana na wataalamu wa ufugaji wa nyuki kutoka TFS Madaba.
Kikundi hicho kipo katika Kata ya Mkongotema na kimesajiliwa kisheria na kinajumla ya watu 19 wanawake 6 na wanaume 13.
Afisa Nyuki wa Halamshauri hiyo Dafroza Kiranda amesema wamefanikiwa kutoa elimu ya ufugaji nyuki utunzaji wa mazingira na jinsi ya kuweka nta kwenye miznga,kutundika mizinga katika matawi ya miti ili kupata makundi ya nyuki pamoja na kufanya ukaguzi na kutunza kumbukumbu za makundi ya nyuki.
Kiranda amesema ufugaji wa nyuki ni tamko lililopo katika ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM ) ikiwa kiongozi wa wa chama ameambatana na wataalamu kutimiza azma ya Ilani ya chama.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halashauri ya Wilaya ya Madaba
Mei 31,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa