Kijiji cha Lituta kimeanza utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini (TASAF) awamu ya tatu Mwaka 2015 utekelezaji wake ulifanyika Halmashauri ya Songea.
Akizungumza Mtendaji wa Kijiji cha Lituta Aisha Nyange amesema kuanzia Mwaka 2020 hadi sasa kijiji cha Lituta kimeendelea kunufaika na shughuri za mpango wa TASAF kwa namna mbalimbali.
Amesema Ikiwa ni pamoja na uhawilishaji wa fedha kama ruzuku kwa walengwa utekelezaji wa miradi ya ajira za mda ,utekelezaji wa Miradi ya Miundombinu na Mpango wa kujenga uwezo kwa ngazi mbalimbali zinazoshiriki katika utekelezaji wa Mpango.
Nyange amesema kaya 78 zilinufaika katika mpango mwaka 2015 hadi sasa kaya 66 zimebaki katika mpango kutokana na baadhi ya walengwa kupua kwa vifo.
Hata hivyo mtendaji amesema kijiji hicho cha Lituta ni moja kati ya vijiji vitatu vilivyopo katika Kata ya Lituta na vingine vinavyounda Kata ni Mtepa na kipingo.
“Kijiji cha Lituta kinajumla ya wananchi 5,039 wanaume 2426 na wanawake 2613 ambapo wenye uwezo wa kufanya kazi 1,192”.
Mtendaji amesema wananchi wa kijiji hicho wanajishughulisha na kilimo cha Mahindi ikiwa kama zao la chakula na maharage,tangawizi na Alizeti kama mazao makuu ya Biashara.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 18,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa