KANISA la Tanzania Assemblies of God Madaba Sehemu ya Ruvuma Kaskazini Jimbo la Ruvuma Kati wameletewa Mchungaji Mpya wa Kanisa la Mahali pamoja Obedi Mwasyika
Mchungaji huyo ameletwa kutokana na Mchungaji Kiongozi aliyekuwa anachunga Kanisa hilo Isaya Mhagama kufariki Machi 10,2023.
Katibu wa Jimbo la Ruvuma Kati Revi Kilatu akimwakilisha Askofu wa Jimbo hilo Joachim Mhanga amemtambulisha katika Kanisa hilo ametoa rai kwa washirika wampokee na kumkubali pamoja na kumpa ushirikiano katika kufanya kazi ya Mungu.
“Tumkubali kama alivyo, tumpe ushirikiano ili tufaidi alichonacho atakuwa Baraka kwetu,maana alijipanga kwenda kuanzisha Kanisa Viongozi wa Juu wamemuona ahudumu Madaba”.
Hata hivyo Kilatu amelipongeza Kanisa hilo kwa ushirikiano waliouonyesha kwa kumjengea Nyumba Mjane wa Mchungaji Isaya Mhagama yenye thamani ya shilingi Milioni 8,442,000/=.
Kwa Upande wake mchungaji huyo mara baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa katika Kanisa hilo amewaomba washirika kumpa ushirikiano katika utendaji wa kazi ya Mungu ili waweze kusonga mbele.
Naye Mwangalizi wa Sehemu ya Ruvuma Kaskazini Islael Mtafya wa Kanisa la Mahanje amesema kuwa anamfahamu Mchungaji Obedi tangia miaka mingi na alianza kufundisha watoto Kanisani huko Mkoani Mbeya.
Mtafya amewaasa washirika hao kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Mchungaji mpya bila kutengeneza makundi ambayo yatasababisha kuharibu Kanisa badala yake kazi ya Bwana iweze Kuimarika.
“Namshukuru Mungu kwaajili ya utulivu na ushirikiano wenu mliouonyesha kuanzia Mchungaji Kiongozi alipo fariki takribani miezi 9 mmekuwa wavumilivu Sana nawapongeza”.
Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo Paulo Motela aliyechunga Kanisa hilo tangia kufariki kwa Mchungaji kiongozi amewashukuru washirika kuanzia Mchungaji Mhagama alipofariki wamempa ushirikiano wakutosha hivyo amesema yupo tayari kufanya kazi chini ya maelezeko ya Mchunga mpya .
“Kuanzia Mchungaji kiongozi alipofariki watu hawa walinithamani sana,kunawakati nilipitia Mazingira magumu walinifariji wakiwemo wazee wa Kanisa na Mwangalizi,hivyo nipo tayari kufanya kazi ya Mungu nikifuata maelekezo yako”.
Imeandaliwa na Aneth ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 26,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa