Kamati ya usimamizi ngazi ya Jamii (CMC) na mafundi viongozi (LSPS) Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamepewa mafunzo ya pamoja katika kutekeleza miradi ya muda mfupi (PWP).
Akifungua Mafunzo hayo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema wametoa mafunzo kwa kamati hizo ili kuhakikisha miradi ya mda mfupi hususani miradi ya vivuko 11 katika vijiji 11 mwaka 2023/2024 vinatarajiwa kujengwa.
Hata hivyo Mohamed ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo hayo kutoa elimu waliyopata katika mafunzo hayo kwa wengine ili waweze kufuata taratibu zote wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
“Niwaombe kupeleka elimu mliyoipata iwafikie wajumbe wengine ili mtakapotekeleza miradi hiyo muweze kufuata taratibu na kanuni zote”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Machi 8,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa