KAMATI ya Siasa Mkoa wa Ruvuma inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Oddo Mwisho imekagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Lilondo Kata ya Wino Halmashauri ya Madaba
Katika Shule hiyo yanajengwa madarasa 8,jengo la utawala maabara ya Fizikia na Baiolojia kwa zaidi ya shilingi Milioni 560 kupitia mradi wa SEQUIP.
Mwisho amezipongeza kamati za ujenzi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Shule hiyo.
“Mimi nimeona Watendaji mnasimamia vizuri mradi huo na kamati zote hata matofari yanayotumika yapo imara kwa kasi mliyonayo naamini mtamaliza kwa wakati”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amemshukuru Rais Samia kwa kuleta fedha za ujenzi wa Miradi mbalimbali katika Halmashauri hiyo zaidi ya Bilioni 5.
“Kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 tumeletewa zaidi ya Bilioni 1 kwaajili ya ujenzi wa shule hii, ukarabati wa Shule ya Msingi Wino na Ifinga Mh.Mwenyekiti tunaomba utufikishie Shukrani zetu za dhati kwa Rais Samia kwa kutulete maendeleo katika Halmashauri ya Madaba”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 7,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa