KAMATI ya Siasa Mkoa wa Ruvuma wamekagua mradi wa vyumba 10 vya madarasa kwa Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Madaba.
Akitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema Halmashauri ya Madaba kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 ilipokea kiasi cha shilingi milioni 2000 kutoka Serikali Kuu kwaajili ya ujenzi wa madarasa 10 katika shule za Sekondari 7.
Amesema shule hizo ni pamoja na Nguluma,Gumbiro,Magingo,Madaba,Mahanje,Wino na Ifinga madarasa hayo yameweza kutatua changamoto ya upungufu wa madarasa kwa wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza 2023.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Nguluma Melksedeck Lwena amesoma taarifa ya ujenzi wa madarasa mawili katika shule hiyo amesema imesajiliwa kwa namba s.1350 na ilianza rasmi Januari 2002 ikiwa shule ya wananchi kata ya Gumbiro kwa sasa inamilikiwa na Serikali na ipo kata ya Mtyangimbole.
Hata hivyo Lwena amesema Octoba 1 ,2022 shule hiyo ilipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 40 kutoka ofisi ya Mkurugenzi kwaajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
“Hadi kufikia Desemba 14,2022 ujenzi ulikamilika kwa asilimia 100 na fedha zote zilizotolewa zilitumika”.
Amesesema manufaa ya mradi huo ikiwa ni pamoja na kupatikana vyumba bora vya madarasa na kuwezesha uandikishaji wa wanafunzi wote 208 waliopangwa kidato cha kwanza 2023.
Kupatikana kwa samani bora kwa wananfunzi wakati wa kujifunza,kupunguza msongamano wa wanafunzi pamoja na kuamsha ari ya wanafunzi wawapo shuleni.
Lwena ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji na upatikanaji wa elimu Nchini.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Februari 2,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa