AFISA Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Anitha Makota amezungumza na wanawake wa jasiriamali wadogo wadogo juu ya uundwaji wa jukwaa la wananwake.
Hayo amezungumza katika Kijiji cha Madaba Kata ya Mahanje amesema jukwaa la wanawake liliundwa kwa lengo la kuwawezesha wajasiriamali wadowadogo kwa kuwapatia fursa ya kujipatia mitaji,masoko pamoja na ushirikiano na Wajasiriamali wengine kutoka sehemu mbalimbali.
“Jukwaa hilo lilianzishwa na Rais Samia akiwa Makamu wa Rais mwaka 20216 alizindua Mkoa wa Dar es Salam Mlimani city na kutoa maagizo ifikapo 2017 Mikoa,Halmashauri,Kata,Mitaa pamoja na vijiji Majukwaa yawe yameundwa”.
Afisa Maendeleo amesema jukwaa la wanawake ni chombo kikubwa kinachowapelekea kukutana na wajasiriamali mbalimbali kutoka Mikoa mingine na Halmashauri tofauti kwa lengo la kujifunza kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.
Hata hivyo amesema jukwaa hilo liliundwa kwa kuwasaidia wanawake kupaza sauti zao mwanzo hawakuwa na sauti ya kuzungumza .
“Nimesikia hapa kuna mama lishe ifike mahali mamalishe ajipatie vyombo vya kisasa hata ikifika wakati wajisikie vizuri kupata huduma katika genge lako”.
Makota amesema lengo lingine lilikuwa maswala ya kujipatia masoko kupitia biashara ndogondogo pamoja na kujipatia elimu ili kuwasaidia wajasirimali kuuza biashara zao ndani na nje.
“Lengo letu ni kuwakutanisha pamoja na wajasiriamali wengine kutoka Wilaya hadi Mikoa mingine kwa kujifunza jinsi gani wao wamefanikiwa”.
Kutoka Kitengengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai 11,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa