HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba Mkoa wa Ruvuma inajumla ya eneo la hekta elfu 37,000 ya kuzalisha biashara ya hewa okaa kupitia kutunza mistu ya asili na uhifadhi wa wanyamapori.
Hayo amesema Afisa Mkuu wa wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii anayesimamia uhifadhi na ushirikishwaji kwa jamii (WMA) Rose Geradi alipozungumza na Jumuiya ya uhifadhi kijiji cha Ifinga katika kikao cha tathimini ya kuangalia nyaraka zilizopo ili iweze kusajiliwa na kuanza kufanya kazi.
“Leo tupo kijiji cha Ifinga kuazisha hifadhi ya wanyamapori jamii tumeangalia tathimini ya awali kama wanakidhi vigezo vya uhifadhi (WMA) ili kukamilisha zoezi la usajili kwa mujibu wa kanuni ya mwaka 2018”.
Hata hivyo Meneja Miradi wa shirika lisilo la kiserikali Honeyguide linalowezesha mafunzo ya Jumuiya za Uhifadhi ukanda wa kusini mwa Tanzania Sylvester Mselle ametoa rai kwa viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa na uongozi bora pamoja na menejimenti na kusimamia utaratibu wa askari watakao linda maeneo.
“Bila uongozi bora hatuwezi kupata wawekezaji wala hatuwezi kujua jinsi ya kuingia mikataba lakini uongozi ukiwa thabiti mtaweza kufuata taratibu na kanuni”.
Mselle amesema shilika hilo linafanya kazi kwa ukaribu na Serikali na linawajengea uwezo jumuiya ili waweze kuwa na uongozi na usimamizi bora ambao utapelekea kulinda rasilimali na kuweza kupata wawekezaji wengi.
Kwa upande wake Afisa wanyamapori Halmashauri ya Madaba Ernest Nombo ameyasema matarajio katika kijiji hicho mara baada ya usajili wa jumuiya hiyo ikiwa kijiji hicho kina hekta 37000 za uhifadhi.
“Baada ya kukamilisha zoezi la usajili wa uhifadhi wananchi watafaidika watakuwa ni sehemu ya usimamizi,watapata fedha kutoka kwenye block,fedha za utalii pamoja na kuwa na askari ambao watakuwa walinzi wa eneo na kupambana na wanyama wakali”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi,11,2024
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa