• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika

IBUGE azitaka Halmashauri kutoa Mikopo ya asilimia 10 kwa Vikundi vya TASAF

Posted on: May 15th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amewaagiza wakurugenzi wa  Halmashauri  zote nane mkoani Ruvumakutoa kipaumbele cha mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa vikundi vya TASAF vinavyofanya vizuri  katika Shughuli za  kiuchumi.

Ametoa maagizo hayo wakati anazungumza katika Kikao kazi cha wadau wa TASAF  kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na kujadili  maendeleo ya mpango wa maendeleo ya TASAFkatika  wa kipindi cha awamu ya tatu  kipindi cha pili.

“Nasisitiza wahusika wote wa utekelezaji wa mpango huu waimarishe uadilifu ,Elimu sahihi kwa walengwa na uwazi katika kutekeleza shuguli zinazohusu upande wa TASAF ili Serikali iweze kufikia malengo yaliyokusudiwa”,alisisitiza RC Ibuge.

Hata hivyo Brigedia Jenerali  Ibuge amewapongeza Waratibu wa TASAF kuanzia ngazi ya Taifa,Mkoa na Halmashauri kwa kuwezesha kutekeleza mpango wa kaya maskini ili waweze kuinuka kiuchumi  ikiwa utekelezaji wa mpango huu umefanyika katika vijiji na mitaa yote ya Mkoa wa Ruvuma 685 na kaya 67,831..

“Nitumie nafasi hii kuwahimiza viongozi wenzangu  wa ngazoi zote washiriki kikamilifu katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za TASAF kwenye maeneo yao ili mpango huu uweze kuwawezesha kaya maskini, watoto na wazee  ambao hawajiwezi  wapate lishe bora,Elimu na afya “.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Mkoa  wa Ruvuma Xsaveria Mlimira amesema Kikao hicho cha wadau wa mradi huo kimeweza   kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi kuwa na utekelezaji wa mpango huu katika   kipindi cha awamu ya tatu kipindi cha pili.

Mlimira ameyataja mafanikio yaliyotokana na Mradi wa TASAF kwa kaya maskini, kuwa ni wanufaika wameweza kukuza kipato cha kaya kupitia biashara ndogondogo kutokana na fedha ya ruzuku,walengwa 18,044 wamejiunga katika vikundi 1290 vya kuweka akiba na kukuza uchumi mkoani Ruvuma..

Amesema asilimia 99 ya walengwa wanatimiza masharti ya elimu na afya, na jumla ya kaya 19,216 wanaoishi maeneo ya vijijini na mjini wamehamasika kujiunga na mhuko wa  afya ya jamii (CHF) ambapo katika Mkoa wa Ruvuma hadi kufikia Mei mwaka huu kaya zaidi ya 24,000 zimejisajiri katika mfuko wa CHF iliyoboreshwa.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Mei 14,2022

 

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA SENSA May 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 10, 2021
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • RC Ibuge azisisitiza Halmashauri kutoa Elimu ya Mikopo

    July 01, 2022
  • SERIKALI yatoa bilioni 1.8 kujenga Hospitali Madaba

    July 01, 2022
  • WALIO husika na ubadhirifu mradi wa Hospitali ya Madaba kuchukuliwa hatua

    June 30, 2022
  • HALMASHAURI zote Ruvuma za pata Hati Safi

    June 29, 2022
  • Angalia zote

Video

RC IBUGE AZISISITIZA HALMASHAURI KUTOA ELIMU YA MIKOPO
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 10

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: info@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa