MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amepiga marufuku wafugaji holela wanaoingia katika Wilaya ya Songea bila kibali.
Hayo amesema alipoongea na wananchi wa Kata ya Mahanje Halmashauri ya Madaba kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa na kuanza kazi rasmi.
“Mfugaji yeyote hata kama amekaa miaka sita kabla mimi sijaingia Songea na alingia bila kibali ataondoka Serikali haishindwi”.
Ndile amesema tangia enzi za Rais wa awamu ya kwanza Hayati Nyerere Songea ilitengwa kwaajili ya kilimo na siyo ufugaji ikiwa Wilaya ambayo inazalisha nafaka na imefanya vizuri kitaifa miaka mine mfululizo.
“Ng’ombe wakiingia na kuanza kukanyaga udongo wanaharibu rutba kwasababu udongo wa Songea ni laini na Ndiomana ikawekwa kwaajili ya kilimo”.
Hata hivyo amesema Mfugaji yeyote lazima aingi na utaratibu na kama kijiji wameridhia na wamekaa mkutano mkuu wakamjadili na kumpa kibali ataruhusiwa ikiwa bado wananchi watahitaji nyama na maziwa.
Mtendaji wa kijiji hicho Jabiri Fussi amesoma taarifa ya kijiji hicho ikiwa na jumala ya kaya 385,jumla ya wakazi 2527.
Fussi ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuchangia shilingi milioni 19 kwaajili ya ujenzi wa zahanati na Mbunge wa jimbo la Madaba milioni 10.
“Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetuunga mkono milioni 225 kwaajili ya mradi wa maji kijiji cha Mahanje”.
Diwani wa Kata ya Mahanje Mheshimiwa Stephano Mahundi amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuchagua kuongea na wananchi wa kijiji hicho kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Februari 3,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa