HALMSHAURI ya Wilaya ya Madaba imeongoza kwa kushika nafasi ya Kwanza ufaulu wa Matokeo ya Darasa la Saba kwa asilimia 87.62 Kimkoa kati ya Halmashauri 8 Mwaka 2023.
Hayo yamesemwa katika Kikao cha tathimini ya matokeo hayo kilicho fanyika katika Shule ya Msingi Madaba na kuhudhuriwa na Waratibu Kata,Wakuu wa Shule,Wataaluma pamoja na Idara ya Elimu ngazi ya Halmashauri.
Afisa Elimu Msingi Saada Chwaya akizungumza katika kikao hicho amewapongea Walimu kwa umoja waliounyesha katika kufundisha na kumaliza mada kwa wakati na kupelekea kuwa wakwanza katika Matokeo ya Darasa la saba Mwaka 2023 Kimkoa.
Hata hivyo Chwaya amewashukuru Walimu kwa usimamiaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ya BOOST,SWASH na kukamilika kwa wakati.
“Tunaboresha Miundombinu yetu siyo kwa Wanafunzi pepekee hata sisi walimu tunapata mazingira mazuri ya kufundishia”.
Kwa upande wake Mratibu Kata ya Matetereka Onyango Nzali akizungumza kwa niaba ya Waratibu Kata amesema ushindi wa Mtihani wa mwaka 2023 umetokana na Wakuu wa Shule na wataaluma kuwa waadilifu na waaminifu na kusababisha kuleta matokeo halisi katika Halmashauri.
“Mtakuwa mashahidi Mtihani wa Utamilifu( Mock) Mkoa tulikuwa wa 8 katika Halmashauri za Mkoa matokeo yalikuwa yetu na yalikuwa halisi kupitia hayo wakuu wa shule na wataaluma mkaona tubadilishe histoaria”.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Wino Talfisius Mapunda akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Shule wa Halmashauri hiyo ameipongeza Idara ya Elimu Msingi kwa Juhudi na kuhakikisha wanaleta umoja kwa Walimu katika Halmashauri ya Madaba na kupelekea kupata matokea mazuri.
“Chamsingi tusimamie taaluma kwa pamoja na mambo mengine yatakuwa salama sisi wakuu wa shule na walimu wote”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Disemba 5,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa