BARAZA Maalum la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Madaba limepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 shilingi Milioni 228,114,000/=.
Akizungmza katika baraza hilo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema kata zitakazopitiwa na mradi wa ujenzi wa Barabara ya kutoka Songea hadi lutukila watapewa fedha shilingi milioni 200 kwaajili ya kuchangia huduma za jamii.
Amesema Kata hizo ni Mtyangimbole,Ngumbiro na Mkongotema ikiwa fedha hizo zitatumika kwaajili ya ujenzi wa miradi katika kata hizo.
“Mheishimiwa Mwenyekiti tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Rais Samia ni mara chache tunaona miradi inajengwa kupitia hiyo tunapata faida kupata miradi mingine”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa katika baraza hilo maalumu amesisitiza suala la umoja na upendo katika utendaji kazi ili kuhakikisha Miradi inayoletwa na Serikali inasimamiwa kwa usahihi.
“Tukipendana hakuta kuwa na kunyosheana vidole hata vitabu vya Mungu vyote vimeandikwa upendo”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 12,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa