• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

Halmashauri ya Madaba Mkoa wa Ruvuma inaardhi yenye rutuba kwa kilimo cha Palachichi

Posted on: December 1st, 2020

Halmashauri ya Wilaya ya Madaba  Mkoa wa Ruvuma inamaeneo mazuri yenye rutuba kwaajili ya kilimo cha mazao ya Biashara na Chakula ikiwemo zao la Palachichi.

Hayo yamesemwa na Afisa kilimo  Umwagiliaji na ushirika (W) zao la  Palachichi linalolimwa  Halamashauri ya Wilaya  ya Madaba huzalisha Tani 281.8 katika eneo la Hekta 192.5.

Mrimi amesema  zao hilo linalolimwa kata ya Mhanje,Lituta,Mateteleka,Wino na Mkongotema na uzalishaji wake ni mchache hivyo wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika maeneo ya Halmashauri hiyo ili kuongeza uzalishaji kwa wingi na ardhi ya Madaba ni nzuri kwa kilimo  ya zao hilo.

“Wananchi wanamwitikio mkubwa kulima zao hilo  na wawekezaji waliopo Silverlands Ndolela Ltd ana hekta 95,Kampuni ya Interfruit na inaendelea kulima zao hilo hekta 1200,Shirika la masister  st Getrude kijiji cha Ndelenyuma  wamepanda jumla ya heka 40 na wakulima wadogo  jumla ya heka 59”. Amesema Mrimi.

Hata hivyo Mrimi amesema zao la Palachichi linastawi katika eneo kubwa la Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kutokana na hali nzuri ya hewa  na udongo wenye rutuba ya kutosha.

‘’Uzalisha wa Zao la Pala chichi eneo la Halmashauri kwa sasa ni mdogo na tunategemea soko la ndani kwa kiasi kikubwa  na kiasi kidogo huuza nje ya Halmashauri”.

Amesema miongoni mwa juhudi wanazoendelea kukuza uzalishaji wa zao hilo Halmashauri inashirikiana na  Taasisi ya Tanzanice,Proganic Tanzania LTD,Ofisi ya Maendeleo Jimbo Katoliki la Njombe,Interfruit,Slverlands Ndolela ltd,Shirika la Masister  st Getrude Ndelenyuma na wakulima wadogo.

Mrimi amesema zao hilo linakabiliwa kuzalishwa kwa uchache kwa sababu hakuna wawekezaji wengi kutoka sehemu zingine isipokuwa ni wenyeji wa Halmashauri hiyo hivyo husababisha uzalishaji kuwa mdogo.

Imeandaliwa  na Aneth Ndonde

Afisa Habari Halmashauri ya Madaba

Desemba 1,2020.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa