• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

HALMASHAURI ya Madaba imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni 126

Posted on: May 12th, 2022

HALMASHAURI ya Madaba Wilaya ya Songea imetoa Mkopo wa Bodaboda 5 kwa kikundi cha Kona Bar zenye thamani ya Shilingi milioni 20.

Akisoma taarifa  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema kwa mwaka wa fedha 2021-20022 wamefanikiwa kutoa mikopo kwa vikundi 20  kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 126.

Mohamed amesema vikundi 7 ni vya wanawake vilikopeshwa zaidi ya shilingi milioni 40,vikundi 8 ni vya vijana vilikopeshwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 74 na vikundi  5 vya watu wenye ulemavu vilikopeshwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 11.

“Tunatarajia kuendelea kutoa mikopo yenye tija kwa makundi maalumu na kusimamia vikundi  kwa kutumia mikopo katika kuzalisha miradi waliyoombea fedha ili kujenga ufanisi mkubwa wa kurejesha mikopo kwa wakati na kupiga hatua ya maendeleo”.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amekuwa mgeni rasmi katika hafla ya ugawaji wa Bodaboda hizo amewaasa wanakikundi hao kutii sheria pamoja na kuwa na Leseni ikiwa Pikipiki hizo zimekatiwa bima kubwa.

Mgema amesema asilimia 10 inayopatikana katika mapato ya ndani ya Halmashauri zitumike vizuri kwa wanawake,watu wenye ulemavu pamoja na vijana ili waweze kutumia na kurejesha kwa wakati iliwengine waweze kupata.

”Mikopo iliyokopeshwa ni milioni 126 kwa Halmashauri ndogo ya Madaba kati ya hizo zingine ni za marejesho ya mwaka uliopita kwa kiwango hiki tunaweza kufikia milioni mia tano za kukopesha”.

Katibu wa Kikundi cha Kona Bar Erasto Filemon ameipongeza Serikali kwa kuwapatia Mkopo huo na ameahidi kusimamia kikundi hicho  kurejesha kwa wakati ikiwa ni mkopo wa pili na kupitia mkopo huo wamepata manufaa kwa kuwainua kimaisha vijana wa Madaba.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Kitengo cha Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Mai 12,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa