HALMASHAURI ya Madaba imetoa taarifa mafanikio ya mpango mkakati wa miaka 5 iliyopita kuanzia 2016-2021 katika hali ya uwekezekaji.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa idara ya Mipango Janeth Nchimbi amesema hali ya uwekezaji wa viwanda katika Halmashauri hiyo hadi kufikia Julai 2021 imekuwa na wawekezaji wakubwa wanne.
Amesema wawekezaji hao wa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula ni Silverland Ndolela African Plantation anafanya shughuli za kilimo cha mazao mchanganyiko hekari 5,000, Wakala wa mistu (TFS) anafanya shughuli ya upandaji miti kwenye eneo la vijiji vya Ifinga,Wino na Mkongotema zaidi ya hekari 24,000
Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Hekta 10,000 Kijiji cha Ifinga wamepanda miti zaidi ya hekta 2,000, Mbangamawe partiners anazalisha chokaa katika kijiji cha Mtyangimbole na Ifinga food processing anaongeza thamani ya mazao kwa kufungasha mazao kama Tangawizi.
Mkuu wa Idara ya mipango amesema mwekezaji wa Kampuni ya Interfruit Limited ya Mjini Songea inatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha matunda ya Parachichi kwenye ardhi ya kijiji cha Mahanje Hekari 3,000 na kujenga kiwanda kwaajili ya kusindika matunda hayo mara yatakapoanza kuvunwa.
“Halmashauri ya Madaba ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya Miti ya mbao,Fito,Nguzo za Umeme,Kahawa,Tangawizi,Matunda mbalimbali kama Parachichi Tangawizi,Mpunga,Mazao ya mafuta (Alizeti,Ufuta na Karanga)”.
Hata hivyo amesema matarajio ya Halmashauri ni kuwapokea wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya kilimo na umwagiliaji ili watumie maeneo mazuri kilimo yaliyopo kwenye eneo la kulima kwenye kiwango kikubwa,pamoja na wawekezaji wa kujenga Viwanada vya kuchakata mazao ya misitu(Miti) na nafaka (Mahindi).
Nchimbi amebainisha maeneo ya uwekezaji yaliyotambulika katika Halmashauri ya Madaba eneo la Hekari 400 lipo kitongoji cha Ifugwe kijiji cha Madaba kilomita 10 kutoka barabara kuu Songea Njombe kwenye Mji wa Madaba ukielekea Wilaya ya Ludewa limetengwa kwaajili ya viwanda mbalimbali.
Eneo la Itombololo Kijiji cha Mkongotema lina hekta 2,000 lipo kandokando ya Barabara kuu ya Songea –Njombe ni eneo lililotengwa kwaajili ya shughuli ya Uwekezaji wa kuchakata na kuongeza thamani ya mazao Tangawizi na Mahindi likiwemo shamba la Mifugo Hekta 4,200(Hekari10,500) ni mali ya Wizara ya Mifugo Halmashauri ya Madaba wanalitunza na kulitumia wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika eneo hilo.
“Halmashauri ya Madaba inamiliki eneo la Hekari 500 lililopo kilomita 18 kutoka barabara kuu Songea –Njombe kuelekea kijiji cha Ifinga lipokwaajili ya mwekezaji yeyote kwa shughuli za kilimo cha Miti,Kahawa na mazao mengine yanayoendana na hayo”.
Madaba inamaporomoko yanayoweza kuzalisha Umeme pamoja na Masigira,Lipupuma na Lingatunda wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika maeneo haya,pamoja na Wiwanja vilivyopo Manispaa ya Songea Plot Na. 285 block “M” Seedferm kipo eneo nzuri kinafaa kwa ujenzi wa Hotel na Majengo yaliyochakaa nyuma ya kanisa Katoliki ambapo Mwekezaji anaweza kujenga kitega uchumi katikati ya Mji wa Songea.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Julai 23,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa