Diwani wa Kata ya Lituta ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Madaba Oraph Pili amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka ulioisha Juni 30 mwaka 2024 kuleta fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Salamu hizo amezitoa katika mkutano maalum wa baraza la Madiwani kuwa katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamepokea fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo afya na elimu.
“Tumepokea fedha kwaajili ya ukamilishaji wa miradi ya afya kipekee tunampongeza kwa ujenzi wa hospitali ya Wilaya iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni tatu”.
Pili amesema katika mwaka ulioisha wamewapongeza wataalam wa halmashauri hiyo kwaajili ya kukusanyaji wa mapato amabyo yamepelekea ukamilishaji wa miradi mbalimbali iliyoanzishwa na wananchi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa