Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Neema Magembe amewapa Elimu ya Ujenzi wa Mradi wa Soko kupitia mradi wa TASAF kamati ya ujenzi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Magembe akizungumza na Kamati hiyo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed kwa kuwaruhusu wataalam pamoja na wanakamati ya ujenzi kwenda kujifunza Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
“ Kujifunza siyo lazima mtoke Madaba na muende Mwanza lakini ndani ya Mkoa wetu kuna Mengi ya kujifunza “.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Songea amewapongeza wataalam hao kwa kuona haja na kwenda kujifunza katika Halamshauri ya Songea juu ya ujenzi wa Soko lililopo Peramiho “A”
“Nasisi tutakuja kujifunza Madaba mnajenga ile EMD pale Hospitali ya Wilaya,tunatarajia tutapokea fedha hivi karibuni tutakuja kujifunza namna ambavyo mmefanikiwa”.
Magembe ametoa rai kwa Kamati ya ujenzi katika Halmashauri hiyo kuhakikisha wanauliza maswali ili waweze kuelewa na kwenda kutekeleza mradi huo kwa umakini na ubora zaidi pamoja na kushikamana katika utekelezaji wa mradi huo.
Amesema mradi unaoenda kujengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ukawe wenye tija na viwango na unaoakisi thamani ya fedha zilizoletwa na Serikali.
“tunaiheshimisha Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetoa fedha hizo”.
Fedha hizo ziwe na matokeo mazuri pamoja na Wabunge wetu Kwetu sisi tunaye Jenista Mhagama akipita na kuona soko hilo anatabasamu,Hivyo hivyo Mbunge wa Madaba Joseph Mhagama mumuheshimishe anahangaika kuhakikisha Madaba mnapata miradi”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 29,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa