MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amewapongeza wakuu wa shule za Sekondari kwa kuongoza Kimkoa kwa matokeo ya kidato cha pili na kidato cha nne mwaka 2023.
Hayo amezungumza katika kikao cha tathimini ya Elimu kilichojumuisha wakuu wa shule za sekondari na kuweka mikakati ya pamoja ya mwaka 2024.
Hata hivyo Mkurugenzi amewataka wakuu wa Shule kutunza mazingira na kubadilishana uzoefu katika taaluma.
“Tujitahidi sana kubadilishana uzoefu mjifunze kwa ambao wamefanya vizuri ikiwemo Sekondari ya wasichana Feo,St Monica na Mahanje Sekondari ili tuweze kufanya vizuri zaidi”.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya wasichana ya Feo Jemaida Erenest amesema kinachopelekea shule hiyo kufanya vizuri mitihani ya kidato cha pili na kidato cha nne ni kuwajengea hofu ya Mungu wanafunzi kila mmoja na dini yake,kumaliza mada kwa wakati,kuwatia moyo walimu na wanafunzi,kutoa motisha kwa walimu pamoja na kufuatilia ratiba zote za walimu.
Naye Mkamu Mkuu wa Shule ya St.Monica Florence Mhuwa amesema mbinu wanazotumia ilikufaulu vizuri wanawapa wanafunzi mitihani ya ndani na nje,kufanya tathimini,kuwasimamia na kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri pamoja na ushindani wa Wanafunzi.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashaui ya Madaba
Machi,01,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa