MKURUGENZI Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amezitaja faida za ujio wa madaktari bingwa katika hospitali ya Wilaya.
Akizungumza akiwa katika hospitali hiyo na kujionea huduma zilizokuwa zinaendelea kutolewa amesema ujio wa madaktari bingwa umepelekea watumishi wa Afya wamepata uzoefu katika utoaji wa huduma kwa wananchi .
“Nitoe wito kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba siku tano zimepita madaktari wetu wataendelea kutoa huduma za kibingwa na mpango wetu tutazindua huduma rasmi zitahusisha katika majengo yaliyopo, Rais Samia ametuletea vifaa vya shilingi milioni 730”.
Amesema vifaa hivyo vimefungwa katika majengo ya hospitali ikiwemo katika vifaa vya kinywa na meno na jengo la mama na mtoto na ni wodi ambazo hazichangamani na wagonjwa wengine pamoja na Exray.
“Namshukuru tena Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia kwa kuendelea kuwajali Watanzania hasa katika huduma za afya ambapo katika awamu hii zimeendelea kuimarika katika halmashauri yetu ya Wilaya,nitoe wito kwa wananchi kuendelea kuitunza miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na baadae".
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 1,2024.a
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa