Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kutoa vifaa kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu (wenye ulemavu).
Mkurugenzi amesema Vifaa hivyo vimeghalimu kiasi cha shilingi Milioni 4,800,000/= na amekabidhi kwa mkuu wa Shule ya Msingi Madaba Victor Luoga hivyo ametoa rai kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa watoto wenye mahitaji maalumu kama ilivyokusudiwa.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 16,2025.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa