MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametoa rai kwa wananchi kujikinga na ugonjwa wa mpox ambao bado hauja ingia katika nchi ya Tanzania.
Akizungumza katika mkutano maalum wa baraza la Madiwani cha kupitisha hesabu za mwisho za Serikali zinazoishia Juni 30,2024 kuwa ugonjwa wa mpox unadalili nyingi ambazo zinapelekea kuambukizwa ikiwemo kula au kugusa mizoga ya wanyama pori, tumbili,Nyani,Sokwe,kugusana na mtu mwenye ugonjwa,kugusa vitu vilivyotumiwa na mtu mwenye ugonjwa,kujamiiana na mtu mwenye ugonjwa,kugusa majimaji ya mtu mwenye ugonjwa.
“Kwa mujibu wa daktari na taarifa aliyotoa tujihadhari kinga ni bora kuliko tiba ugonywa huo unaambukizwa kwa njia nyingi kwa sasa umefika nchi ya Burundi na umetangazwa ni janga la Taifa”.
Dalili za ugonjwa wa mpox ni kupata upele,malengelenge au vidonda kwenye mwili hasa mikononi na miguuni,kifuani,usoni na sehemu za siri.
Aidha amesema jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo kuepuka kugusa majimaji ya mwili ya mtu mwenye mpox,kuepuka kukumbatiana na kubusiana,kushikana mikono na mtu mwenye mpox.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa