Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametoamotisha katika Shule za Msingi kwa kufanya vizuri matokeo ya darasa la nne na darasa la saba mwaka 2023.
Mkuu wa Idara ya Elimu msingi Saada Chwaya akimwakilisha Mkurugenzi katika shule hizo 30 ikiwa shule za Serikali 29 na binafsi 1 ametoa kilo 10 za sukari na majani pakti 2 kwa kila shule yenye thamani ya shilingi 1,500,000/=kwaajili ya chai ya walimu wawapo shuleni.
“Naomba tuendelee kung’ara kuna shule zingine sikutegemea kupitia kufanya kwenu vizuri mmeona tumepata na madarasa mazuri karibia kila shule, matokeo yaendane na majengo yake mazuri tuliyopewa kwa moyo wa dhati kabisa niwapongeze sana”.
Hata hivyo amesema Halmashauri ya Madaba imekuwa ya kwanza Kimkoa na kitaifa kati ya Halmshauri 184 halmashauri 68 zimefikia kigezo cha kitaifa cha asilimi 85 halmshauri ya madaba ni miongoni.
“Mmetuheshimisha viongozi wa Halmashauri tumeona tuwashike mkono mnapokuwa mnawasaidia vijana wetu sukari hii tunajua kila mwali atatumia bila kuangalia mwalimu mmoja mmoja”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 14,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa